• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapaka matope China kabla ya waziri wake wa mambo ya nje kufanya ziara nchini China

    (GMT+08:00) 2018-10-05 20:03:10

    Makamu rais wa Marekani Mike Pence jana amehutubia jopo la washauri bingwa mjini Washington na kusema China imeingilia mambo ya ndani na uchaguzi utakaofanyika nchini Marekani, na pia ametoa lawama kwa China katika masuala ya Taiwan, Bahari ya Kusini na haki za binadamu. Kauli hii imepingwa vikali na wizara ya mambo ya nje ya China.

    Bw. Pence amesema hayo kabla ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani nchini China ambayo inatarajiwa kuanza jumatatu wiki ijayo. Katika ziara hiyo, pande hizo mbili zitabadilishana maoni kuhusu masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa nazo.

    Marekani ina kawaida ya kuilaani China wakati inapofanya mazungumzo na China, na katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, Marekani imefanya hivyo mara nyingi katika suala la biashara, ili kutafuta faida kubwa zaidi.

    Lakini ukweli ni kwamba, China haipendi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, kwani ina kanuni ya kidiplomasia ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, pia inajishughulisha na maendeleo ya uchumi na jamii yake. Hata waziri wa usalama wa ardhi wa Marekani Kirstjen Nielse amesema, hakuna ushahidi unaoweza kuthibitisha kuwa China inajaribu kuathiri uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2018. Wizara ya mambo ya nje ya China imesema, jumuiya ya kimataifa inafahamu vizuri nchi gani inapenda kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine mara kwa mara.

    Ingawa mkwaruzano wa kibiashara kati ya China na Marekani umeongezeka tangu Donald Trump awe rais wa Marekani, lakini mwaka jana thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia dola bilioni 583.7 za kimarekani. Aidha, zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Marekani zinapaswa kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kimataifa, yakiwemo mapambano dhidi ya ugaidi, mtandao wa Internet, anga ya juu, na vita.

    Mtafiti wa taasisi ya Brookings Bw. Jeffrey Bader, ambaye alikuwa mkurugenzi wa idara ya mambo ya Asia ya Kamati ya Usalama ya Marekani hivi karibuni amesema, kama serikali ya rais Trump haitarekebisha msimamo wake, na kujitoa na uhusiano na China katika mambo ya maendeleo, italeta athari kubwa kwa Marekani.

    Bila kujali mabadiliko ya sera ya Marekani, sera ya China kuhusu Marekani ni dhahiri na ya siku zote, yaani kutopingana, kuheshimiana na kushirikiana, ili kupata mafanikio ya pamoja. Ikiwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, Marekani inapaswa kusikiliza maoni sahihi, na kujifunza kuheshimu nchi nyingine kwanza, ili iwe nchi ya kuheshimiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako