• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha Nchi za Kusini chasema kipengele cha 301 cha sheria ya Marekani kinakiuka utaratibu wa WTO

    (GMT+08:00) 2018-10-06 18:42:37

    Kituo cha Nchi za Kusini hivi karibuni huko Geneva kimetoa ripoti, ikisema kipengele cha 301 cha sheria ya Marekani kinakiuka utaratibu wa Shirika la Biashara Duniani WTO, kinaharibu kanuni ya pande nyingi na kuleta athari mbaya kwa uchumi wa dunia.

    Kituo cha Nchi za Kusini kilianzishwa mwaka 1995, na nchi wanachama 54 zote ni nchi zinazoendelea. Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Carlos Maria Correa amesema, ukaguzi uliofanywa na Marekani kwa mujibu wa kipengele cha 301 cha sheria ya nchi hiyo umefuata vigezo vyake yenyewe badala ya vigezo vya WTO, na hatua zilizochukuliwa kutokana na ukaguzi huo ni tishio dhidi ya mfumo wa biashara wa pande nyingi.

    Aidha Bw. Carlos amesema, sababu ya Marekani ya kuchukua hatua dhidi ya China si ya kibiashara, ni kutaka kuzuia China kuishinda Marekani katika kasi ya maendeleo ya viwanda na tekenolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako