• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hadi kufikia mwezi Septemba wafanyakazi 8 wa kutoa misaada wameuawa na wengine 12 wakijeruhiwa nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-10-06 18:48:47

    Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa kutoa misaada wanaofanya shughuli zao nchi Somalia yamesababisha vifo vya takribani watu saba na kujeruhi wengine 12 katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia haki za binadamu OCHA, takribani vitendo 90 vya vurugu vimetekelezwa dhidi ya asasi za kutoa huduma za kibinadamu, ikiwemo utekaji wa watu 18 na vifungo, na wengine 13 kuwekwa kizuizini.

    Aidha kutokana na mashambulizi ya kigaidi kwenye maeneo yenye watu wengi mjini Mogadishu kumeendelea kuwa chanzo cha vifo vya wengi na wengine wakijeruhiwa, pamoja na kusababisha uharibifu wa maeneo ya watu na mali zao.

    OCHA imelaani vitendo vya vurugu vinavyoathiri shughuli za asasi zinazotoa misaada ya kibinadamu na kuitaja nchi hiyo kuwa moja ya nchi zilizo ngumu kufikiwa na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako