• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Sudan Kusini zakubaliana kuimarisha amani mpakani, na kuufungua mpaka huo

    (GMT+08:00) 2018-10-06 19:19:47

    Shirika la habari za Sudan SUNA limeripoti kuwa Sudana na Sudan Kusini zimekubaliana kuimarisha amani katika eneo la mpakani, na kuondoa vizuizi, na kufungua milango ya kuingia na kutoka kabla ya kuisha kwa mwaka 2018.

    Sudan a Sudani Kusini jana ijumaa zimehitimisha mazungumzo ya kijeshi, ambapo wanadhimu wakuu wa majeshi ya nchi hizo mbili walitiliana saini mazungumzo hayo na baadaye kuyathibitisha kuwa makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi.

    Mnadhimu mkuu wa majeshi ya Sudan Abdul-Marouf Al-Mahi amesema mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili na kuziwezesha pande mbili hizo kukabiliana kwa pamoja kwenye masuala muhimu.

    Kwa upande wake Gabriel Jok Riak ambaye ni mnadhimu mkuu wa jeshi la Sudan Kusini alirudia kusema msimamo kamili wa nchi yake katika makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako