• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya awataka viongozi kuacha kushindana wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2018-10-07 18:47:54

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana ametoa wito kwa viongozi wa nchi hiyo kuacha siasa zisizo za lazima na badala yake waangazie katika maendeleo ili kuinua kiwango cha maisha ya wakenya.

    Akizungumza wakati wa zoezi la kufanya usafi mjini Nairobi, Kenyatta aliwataka viongozi kupunguza ushindani wa kisiasa na hivyo waache kusababisha tofauti zisizohitajika wakati huu ambapo wakenya wanahitaji kupata maendeleo.

    Kenyatta pia alisema ni muhimu kuheshimiana kwa misingi ya vyama na akikumbusha kuwa hakuna maendeleo yatakayopatikana kutoka chama kimoja bila kushirikiana kama nchi moja, akisisitiza kuwa muda wa ushindani ni vyema ukawa kila unapofika wakati wa uchaguzi.

    Jana Rais Uhuru Kenyatta aliungana na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya mazingira Erik Solheim pamoja na Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia makazi Bw. Viktor Kisob, katika zoezi la kusafisha eneo la soko la uhuru mjini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako