• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan na Marekani zakubaliana kufanya ushirikiano kuhusu suala la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-10-07 18:48:57

    Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe tarehe 6 alasiri kwenye ikulu yake alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo. Wawili hao walibadilishana maoni kuhusu suala la Korea Kaskazini na kukubaliana kufanya ushirikiano kuhusu masuala husika.

    Bw. Pompeo tarehe 7 atafanya ziara nchini Korea Kaskazini. Bw. Abe na Bw. Pompeo siku hiyo walibadilishana maoni kuhusu majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini. Bw. Abe alisema kuwa Japan inataka kufanya majadiliano na Marekani kuhusu suala la silaha za nyuklia la Korea Kaskazini na suala la kutekwa nyara wajapani na Korea Kaskazini.

    Pande hizo mbili pia zilithibitisha kuendelea kutekeleza azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo, na kufikia makubaliano kuhusu kufanya ushirikiano kati ya Japan, Marekani na Korea Kusini kwa ajili ya kuifanya Korea Kaskazini kuchukua hatua halisi ya kutokuwa na silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako