• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yateuliwa kuandaa mkutano mkuu wa shirikisho la michezo ya jumuiya ya madola 2019

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:13:01

    Kamati kuu ya michezo ya jumuiya ya madola imethibitisha kuwa nchi ya Rwanda itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho la michezo ya jumuiya ya madola CGF utakaofanyika mwakani mwezi Septemba.

    Mkutano huo utafanyika mjini Kigali na utatumika pia kuadhimisha miaka 10 tangu taifa la Rwanda lijiunge na michezo ya Jumuiya ya Madola.

    Hii ni mara ya pili kwa mkutano huo kufanyika barani Afrika, mara ya mwisho ulifanyika mjini Kampala nchini Uganda mwaka 2012.

    Katika hatua nyingine taifa la Rwanda, limeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako