• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: FIFA yaisimamisha uananchama Sierra Leone

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:13:19

    Shirikisho la Soka duniani (FIFA) limeisimamisha uanachama Sierra Leone kufuatia Serikali ya nchi hiyo kuingilia shughuli za uendeshaji wa Chama cha Soka SLFA.

    Hatua hiyo inakuja baada ya Tume ya Kuzuia Rushwa kuwaondoa madarakani, Rais wa SLFA Isha Johansen na Katibu Mkuu wake, Christopher Kamara.

    Iwapo kifungo hicho hakitatenguliwa hii ina maana kuwa mechi mbili za Oktoba 11 na marudio Oktoba 15 kati ya Sierra Leone na Ghana za kufuzu Afcon mwaka 2019 zitafutwa.

    Sierra Leone ni miongoni mwa timu nne zenye pointi tatu katika Kundi F, ambalo linahusisha pia timu za Ethiopia na Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako