• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetesi za Usajili: Wachezaji na Makocha

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:13:55

    Habari moja kutoka gazeti la Sunday Mirror la nchini Uingereza inaeleza kuwa Zinedine Zidane amepigiwa simu ya kumtaka asipokee ofa kufundisha timu yoyote kwa hivi sasa, kwani kuna uwezekano akaajiriwa na Manchester United ambayo wingu zito limetanda dhidi ya kocha wa sasa Jose Mourinho.

    Kwingineko katika gazeti la The Mail on Sunday kuna habari inayosema klabu ya Aston Villa imefanya mazungumzo na Thierry Henry kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

    Nako nchini Ujerumani, kufuatia rekodi mbaya ya vipigo mfululizo iliyopata timu yake, imeripotiwa kuwa kocha mkuu wa Bayern Munich Niko Kovac sasa kibarua chake kipo mbioni kuota nyasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako