• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha, Brigid Kosgei ashinda mbio za marathoni za Chicago

  (GMT+08:00) 2018-10-08 09:18:38

  Mwanariadha Brigid Kosgei wa Kenya, jana ameshinda mbio za marathoni za Chicago kwa kuandika rekodi binafsi ya kwake mwenyewe alipotumia saa 2 dakika 18 na sekunde 35, tofauti na mwaka jana katika mbio kama hizo alipotumia saa 2 dakika 20 na sekunde 13 nyuma ya Tinuresh Dibaba wa Ethiopia.

  Nafasi ya pili katika mbio za mwaka huu za Chicago ilikamatwa na Roza Dereje wa Ethiopia, na nafasi ya tatu pia ikienda kwa MuEthiopia Shure Demise.

  Kwa upande wa wanaume, bingwa wa mbio hizo alikuwa ni Mo Farah wa Uingereza aliyetumia saa 2 dakika 8 na sekunde 11, na mshindi wa pili akiwa ni Mosinet Geremew wa Ethiopia na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Suguru Osako wa Japan.

  Kenneth Kipkemoi wa Kenya alishika nafasi ya nne kwa kutumia saa 2 dakika 5 na sekunde 57.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako