• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Pompeo na Kim wafanya mazungumzo "ya kiujenzi" mjini Pyongyang

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:22:18

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un wamefanya mazungumzo "ya kiujenzi" Jumapili mjini Pyongyang.

    Msemaji wa wizara hiyo Bibi Heather Nauert amesema kupitia taarifa kuwa, Bw. Pompeo na Bw. Kim wamejadili mambo manne yaliyoko kwenye Taarifa ya pamoja ya Singapore iliyotolewa baada ya marais wa Marekani na Korea Kaskazini kukutana mwezi Juni, na pia wamebadilishana maoni kuhusu mpango wa mkutano wa pili kati ya marais wa nchi hizo mbili.

    Baada ya kukamilisha ziara yake nchini Korea Kaskazini, jana Bw. Pompeo aliwasili Seoul na kukutana na rais na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, ili kuwaarifu kuhusu ziara yake nchini Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako