• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wachache wajitokeza kupiga kura kusini magharibi katika uchaguzi mkuu wa Cameroon

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:22:43

    Tume ya uchaguzi ya Cameroon imesema wapiga kura walikuwa na uhofu wa kupiga kura zao kwenye maeneo ya kusini magharibi yanayotumia lugha ya Kiingereza, kutokana na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji ambao wanajaribu kuanzisha nchi iitwayo "Ambazonia".

    Mjumbe wa tume ya uchaguzi ya Cameroon Bw. Divine Mewanu Mokoto amesema zaidi ya 90 ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa, lakini wapiga kura walikuwa ni wachache, baada ya wapiganaji kushambulia vituo hivyo.

    Amesema kwenye maeneo ya kaskazini magharibi ambayo ni kanda nyingine nchini humo inayotumia lugha ya Kiingereza, zoezi la upigaji kura pia lilifanyika kwenye mazingira yenye utatanishi, ambapo vikosi vya serikali viliwaua wapiganaji wawili waliojaribu kuvuruga uchaguzi.

    Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Cameroon, watu milioni 6.6 walijitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa Jumapili, na matokeo yatatangazwa na Baraza la katiba ndani ya siku 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako