• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia azindua eneo maalum la viwanda lililojengwa na China

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:35:28

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed, amezindua eneo la viwanda la Adama, lililoko kilometa 74 kusini mwa mji wa Addis Ababa.

    Eneo hilo lililojengwa na kampuni ya uhandisi na ujenzi ya China CCECC, ni sehemu ya juhudi za serikali ya Ethiopia kubadilisha uchumi, kutoka uchumi wa kilimo kuwa uchumi wa viwanda.

    Eneo hilo lililosanifiwa na kujengwa kwa vigezo vya kimataifa, kwenye eneo la hekta 100 kwa gharama za dola za kimarekani milioni 146, linatarajiwa kuleta nafasi elfu 25 za ajira kwa waethiopia.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa eneo hilo, Bw. Ahmed amelitaja eneo hilo kama ni muhimu kwa mahitaji ya maendeleo ya viwanda ya Ethiopia, na kitimiza utoaji wa ajira kwa waethiopia waliohitimu masomo. Amesema mageuzi ya kisiasa yaliyokuwa yanafanyika nchini Ethiopia tangu mwezi April sasa yamekamilika, na mkazo sasa unaelekezwa kwenye mahitaji ya kiuchumi ya wananchi milioni 150 wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako