• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana yaangalia soko la China kwa ajili ya bidhaa zake za nyama

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:35:55

    Batswana inaangalia uwezekano wa kuuza nyama na bidhaa zake kwenye soko la China, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuhimiza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi.

    Akiongea na wafugaji mjini Francistown, waziri wa maendeleo ya kilimo na usalama wa chakula wa nchi hiyo Bw. Patrick Ralotsia amesema serikali ya Botswana inaangalia njia za kupanua uuzaji wa nyama nje ya nchi. Kwa sasa nchi hiyo inazalisha tani elfu 24 za nyama.

    Botswana imekuwa ikitafuta fursa ya kuuza nyama yake kwenye soko la China kwa muda sasa, na tayari imeomba kibali cha kuingiza nyama kwenye soko la China ili kuanza kuuza nyama kwenye soko hilo. Kwa mujibu wa kituo cha uwekezaji na biashara cha Botswana, bidhaa za nchi hiyo zinazouzwa zaidi nchini China ni almasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako