• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kufufua mji mkongwe kwa ajili ya kuhimiza sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2018-10-08 09:51:38

    Mamlaka ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro imesema inaanza kazi ya kujenga upya mji mkongwe uliozikwa chini ya bonde la Engaruka kwenye eneo la Monduli, kwa lengo la kuhimiza sekta ya utalii kwenye eneo maalum la kujiolojia lililozinduliwa hivi karibuni.

    Ofisa wa mamlaka hiyo Bw. John Pareso amesema kazi ya kuchimba, kukarabati na kulinda mabaki ya miundo ya mawe ya zamani ambayo yanakadiriwa kuwa ni mji wenye historia ya miaka 800 wa Engaruka zimeanza hivi karibuni kwenye eneo la Ngorongoro-Lengai.

    Tanzania ikiungwa mkono na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la umoja wa mataifa UNIESCO, inafanya kazi ya kufufua eneo hilo la mabaki, ambalo katika siku za karibuni limeanza kuvutia watafiti, wanataaluma na watalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako