• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini na Marekani zakubaliana kufanya mkutano wa pili wa kilele hivi karibuni

    (GMT+08:00) 2018-10-08 16:53:22

    Korea Kaskazini na Marekani zimekubaliana kufanya majadiliano zaidi kwa ajili ya mkutano wa pili wa kilele kati ya nchi hizo hivi karibuni.

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ambaye yuko ziarani nchini humo wametoa ahadi hiyo jana mjini Pyongyang.

    Kim Jong Un amesema, maendeleo yanaonekana katika kutekeleza taarifa ya pamoja iliyotolewa Juni 12 katika mkutano wa kwanza kati ya Marekani na Korea Kaskazini. Pia amesema anaamini kuwa majadiliano na mazungumzo kati ya nchi hizo mbili yataendelea katika mwelekeo chanya katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako