• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zatakiwa kushikilia ushirikiano wa kunufaishana na kutopambana

    (GMT+08:00) 2018-10-08 17:11:13

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Wang Yi amesema, hivi karibuni Marekani ilizidisha mgogoro wa biashara kwa China, na wakati huo huo, ilichukua hatua mfululizo za kuharibu haki na maslahi ya China kwenye suala la Taiwan. Pia amesema Marekani ilikosoa sera za ndani na za nje nchini China bila ya msingi wowote, vitendo ambavyo vimeharibu uaminifu wa nchi hizo mbili, pia kutoendana na maslahi ya wananchi wao. Amesema China inatetea kuwa China na Marekani zinapaswa kushikilia njia ya kufanya ushirikiano wa kunufaishana, na kutopambana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako