• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika waridhishwa na uchaguzi wa rais nchini Cameroon

    (GMT+08:00) 2018-10-08 18:25:48

    Umoja wa Afrika umeeleza kuridhishwa na jinsi uchaguzi wa rais nchini Cameroon ulivyofanyika.

    Kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi ya Umoja huo Kwesi Ahoomey-Zunu amesema, uchaguzi huo uliofanyika jana ulifanyika vizuri, na kwamba ingawa hana tathmini kamili ya jinsi uchaguzi ulivyofanyika, taarifa alizopata zimeeleza kuwa hali haikuwa nzuri sana katika maeneo yanayotumia lugha ya kiingereza.

    Tume ya Uchaguzi ya Cameroon imesema matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa na Tume ya Katiba ndani ya siku 15 baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika.

    Watu milioni 6.6 walijitokeza kupiga kura jana licha ya mvutano mkubwa katika maeneo mawili yanayozungumza kiingereza, ambako makundi yenye silaha yanapigana kujitenga ili kuanzishwa nchi mpya iitwayo "Ambazonia".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako