• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kupanda kwa kiwango cha matumizi ya fedha kwa watalii wa China kwaonesha imani juu ya mustakabali wao

  (GMT+08:00) 2018-10-08 18:36:36

  Kutalii ni shughuli muhimu zinazofanywa na wachina wakati wa mapumziko ya Siku ya Taifa. Takwimu mpya zimeonesha kuwa, mwaka huu sehemu zenye vivutio vya kiutamaduni zimevutia zaidi watalii wa China, huku kiwango cha matumizi ya fedha cha watalii katika nchi za nje pia kikiinuka. Wataalamu wanaona hali hii imeonesha imani kubwa ya wachina juu ya utamaduni wa kichina na mustakabali wa taifa.

  Wakati wa mapumziko ya Siku ya Taifa, watalii wengi walitembelea maeneo ya mabaki ya kale na makumbusho ya kihistoria ili kupata ufahamu wa kina kuhusu utamaduni wa kale wa kichina. Ikilinganishwa na njia ya kusafiri na kupiga picha katika miaka mingi iliyopita, hivi sasa watalii wengi wanazingatia kupata ufahamu wa kina. Bibi Peng aliyetalii mkoani Hubei wakati wa siku za mapumziko anasema:

  "Wakati wa siku za mapumziko, nilienda mjini Wuhan na Jingzhou, mkoani Hubei, nilijisikia vizuri sana! Kumbukumbu kubwa niliyobaki nayo ni kwamba, hii ni sehemu iliyokuwepo Dola la Chu wakati wa enzi ya kale, wakati kengele ya Bianzhong ikipigwa, taswira ya Dola ya Chu ilinijia kichwani. Nilipopanda kwenye ghorofa ya juu ya Huanghelou, mandhari nzuri ya mto Changjiang ilikuwa ikionekana, hali ambayo imenikumbusha mashairi maarufu ya Cui Hao na Li Bai, ambayo yananifurahisha sana."

  Takwimu kutoka Tovuti ya utalii ya Tuniu zimeonesha kuwa, nchi kumi za mwanzo zilizovutia zaidi watalii wa China ni pamoja na Ufaransa, Italia, Uswisi, Ujerumani, Russia, Marekani, Uturuki, Austria, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Czech. Mkuu wa Idara ya uhusiano na nje ya Tovuti ya Utalii ya Tuniu Bibi Zhao Shuang anasema:

  "Kutokana na Mashindano ya Soka ya Kombe la Dunia, watalii wengi walienda Russia kabla ya Siku ya mapumziko, wengine wanachagua 'safari ya siku 10 za Uturuki', na 'safari ya 15 za Misri na Uturuki'."

  Takwimu pia zimeonesha kuwa, watalii wengi walilipa kwa njia ya simu, maeneo ya matumizi ya fedha katika nje za nje yamepanuka kutoka Asia hadi Ulaya na kuenea kote duniani. Wakati huo huo fedha za watalii za China zinatumiwa zaidi kupata uzoefu wa kuishi pamoja na wenyeji badala ya kununua vitu.

  Mtafiti wa Taasisi ya fedha ya Chongyang katika Chuo Kikuu cha Renmin cha China Bw. Bian Yongzu, anaona hali hii imeonesha kuwa watu wengi zaidi wanatafuta mahitaji ya kirohoi, na pia imeonesha wachina wana imani kubwa zaidi utamaduni wa jadi wa China, na mustakabali wa nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako