• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ngazi ya matumizi yaanza kuongezeka nchini China

    (GMT+08:00) 2018-10-08 19:03:59

    Takwimu zilizotolewa na kituo cha takwimu cha utamaduni na utalii cha China zimeonyesha kuwa, katika siku za mapumziko za Siku ya Taifa mwaka huu, sehemu mbalimbali za China zimewapokea watalii milioni 726, ambayo imeongezeka kwa asilimia 9.43. Pato la utalii wa ndani limefikia dola bilioni 86.5 za kimarekani ambalo linaongezeka kwa asilimia 9.04 ikilinganishwa la mwaka jana. Mbali na hayo, idadi ya wachina waliotalii katika nchi za nje ikifikia milioni 7, ambapo China imeshika nafasi ya kwanza kwa miaka mitano mfululizo katika nchi zenye watu wengi zaidi wanaotalii nchi za nje.

    Ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita, matumizi ya bidhaa na huduma nchini China yameonesha mwelekeo wa kupanda ngazi. Wachina wameingia katika zama ya kupanda ngazi ya matumizi ambayo inazingitia zaidi sifa, hisia na tofauti ya huduma anayopatiwa kila mteja.

    Kupanda kwa ngazi ya matumizi kunategemea bidhaa na huduma zenye sifa nzuri. Tangu mwaka 2015 ambapo China iliimarisha mageuzi ya utaratibu wa uchumi, utaratibu wa bidhaa za China unaendelea kuboreshwa. Hususan tangu mwezi Julai China ipunguze ushuru wa kuagiza bidhaa zaidi ya aina 1,449 za matumizi ya kila siku, wateja wa China wamepata machaguo mengi zaidi. Kwa mujibu wa jukwaa la biashara ya kielektroniki la China, katika siku za mapumziko za Siku ya Taifa, bidhaa zilizonunuliwa na wachina zimeonesha mwelekeo wa kiwango cha juu, ambazo ni pamoja na televisheni zenye skrini kubwa, mashine ya kufua na kukausha nguo, mashine ya kutafsiri, roboti ya kusafisha sakafu pamoja na roboti ya kucheza na watoto.

    Katika siku za baadaye, manufaa mengi zaidi yatapatikana nchini China. Kuanzia Novemba Mosi, China itapunguza ushuru dhidi ya bidhaa za aina 1,585 ambazo zinahusisha bidhaa nyingi zinazohitajika katika uzalishaji wa kampuni na maisha ya watu. Maonesho ya kwanza ya manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya China yatafanyika Novemba 5 huko Shanghai, ambayo yanatarajiwa kuvutia wafanyabishara zaidi ya laki 1.5 kutoka nchi na sehemu 130. Wakati huohuo, serikali ya China inapanga duru mpya ya kupunguza ushuru na gharama. Hayo yote yataleta manufaa kwa wachina wanaotafuta maisha mazuri zaidi, na pia yataleta nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi wa China yenye sifa nzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako