Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa baada ya Jopo la Kati ya Serikali kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa IPCC kutoa ripoti ikitaka ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzi 1.5. Ripoti hiyo imesema kutimiza lengo la nyuzi 1.5 badala ya nyuzi 2 iliyokubaliwa kwenye Makubaliano ya Paris kutatoa manufaa kwa watu na mifumo ya kiikolojia ya asili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |