• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kiongozi wa kamati ya TFF ajiuzulu wadhifa wake

    (GMT+08:00) 2018-10-09 08:50:28

    Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, Revocatus Kuuli amejiuzulu nafasi yake.

    Hata hivyo TFF imesema shughuli za kamati hiyo zitaendelea kama kawaida licha ya kiongozi huyo kujiuzulu.

    Katika maelezo yake Kuuli alisema hawezi kuongoza kamati ikiwa anaingiliwa katika majukumu yake na uongozi wa TFF.

    Inadaiwa kuwa TFF ilimtaka Kuuli aandike barua ndani ya siku tatu ya kujieleza ni kwa nini amesimamisha uchaguzi ndani ya klabu ya Simba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako