• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Samwel Etoo: Kutua Tanzania kesho

    (GMT+08:00) 2018-10-09 08:50:46

    Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon, Samuel Eto'o Phills anatarajia kutua nchini Tanzania kesho Jumatano kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu utakaokuwa unamilikiwa na kampuni ya bia ya Tanzania TBL.

    Mbali na kuzindua uwanja huo, Eto'o ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Chelsea ya Uingereza na Barcelona ya Hispania kwa nyakati tofauti atashiriki kuhamasisha vijana kuhusu michezo nchini humo.

    Michezo ya Olimpiki ya Vijana: Senegal wenyeji mwaka 2022

    Taifa la Senegal limeteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya vijana ya majira ya joto kwa mwaka 2022.

    Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika barani Afrika, yakiwa yamefanyika tayari kwa awamu tatu nje ya bara hilo.

    Akiwatangaza Senegal, Rais wa michezo ya Olimpiki Thomas Bach, alisema lengo la kuichagua Afrika awamu hii ni kwa sababu ya vipaji vingi vinavyopatikana katika bara hilo.

    Mashindano ya Olimpiki kwa vijana ya mwaka yanaendelea nchini Argentina yalianza Oktoba 1 na yanatarajiwa kumalizika Oktoba 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako