• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihimiza Marekani kusitisha hatua za kuharibu maslahi yake

    (GMT+08:00) 2018-10-09 09:15:22

    China imeihimiza Marekani kusitisha mara moja hatua za kuharibu maslahi yake, na kutoa wito kwa nchi hizo mbili kufuata njia sahihi ya ushirikiano wa kunufaishana, badala ya kuelekea kwenye mgogoro na makabiliano.

    Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kamisheni ya mambo ya nje ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Yang Jiechi, alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ambaye yuko ziarani nchini China.

    Bw. Yang Jiechi amesisitiza kuwa China italinda kithabiti mamlaka, usalama na maslahi yake, na pia ametoa mwito kwa Marekani kufanya uamuzi sahihi, kwenda sambamba na China na kutekeleza kwa makini makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili katika mikutano iliyopita kati yao.

    Kwa upande wake Bw. Pompeo amesema Marekani inapenda kuimarisha mawasiliano na China na kutafuta mpango wa kiujenzi, ili kutatua changamoto zinazoukabili uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako