• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yauza dhamana za serikali zenye thamani ya dola milioni 400 ili kuunga mkono bajeti

    (GMT+08:00) 2018-10-09 09:36:44

    Kenya imezua dhamana za serikali zenye thamani ya dola milioni 400, ili kuunga mkono bajeti, wakati kukiwa na ongezeko la ununuzi wa dhamana za serikali kutoka kwa wawekezaji.

    Benki Kuu ya Kenya imesema dhamana hizo ni za muda wa miaka 15, zitakuwa na faida ya asilimia 12.8, na zitauzwa hadi tarehe 16 mwezi huu, na mkupuo wa pili utaanza tarehe 23 mwezi huu.

    Habari nyingine kutoka Kenya zinasema Benki ya dunia na shirika la utafiti wa kilimo na mifugo, wamezindua jukwaa la ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa. Mchumi mwandamizi wa benki hiyo Bw. Ladisy Chengula, amesema jukwaa hilo lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 100 litawasaidia maofisa wa Kenya kutabiri mvua au ukame, na kuwaarifu mapema wakulima ili kuepuka hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako