• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi ya internet nchini Rwanda yaongezeka kwa asilimia 25

    (GMT+08:00) 2018-10-09 09:37:02

    Idadi ya watu wanaotumia internet nchini Rwanda imeongezeka kwa asilimia 25 katika mwaka wa fedha uliopita na kuishia mwezi Juni. Mamlaka ya usimamizi wa mtandao wa internet imesema idadi ya watu waliomba huduma hiyo imeongezeka kutoka milioni 4.3 hadi milioni 5.4.

    Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu matumizi ya internet nchini Rwanda yalifikia asilimia 46.6, na ongezeko la matumizi ya internet limetokana na watu kuwa na uwezo wa kumudu gharama za simu aina ya smartphone.

    Mbali na matumizi ya internet kuongezeka, matumizi ya simu za mkononi pia yameendelea kuongezeka, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, idadi ya watumia simu za mkononi iliongezeka kutoka watu milioni 8.8 hadi milioni 9.2, likiwa ni ongezeko la asilimia 4.6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako