• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Cameroon yakanusha madai ya ushindi ya mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2018-10-09 09:56:32

    Waziri wa utawala wa taifa wa Cameroon Bw. Pal Atanga Nji, amesema ni kinyume na katiba kwa mgombea yeyote kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 7 mwezi Oktoba.

    Bw. Nji amesema ni tume ya katiba tu ndio yenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

    Bw. Nji alisema hayo baada ya mgombea wa upinzani Bw. Maurice Kamto, kujitangaza kuwa mshindi kwenye uchaguzi wa urais. Bw. Kamto aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wananchi wa Cameroon wamempa mamlaka ambayo ataitetea kwa nguvu hadi mwisho..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako