Akihutubia mkutano wa 8 wa maadhimisho ya Desmond Tutu uliofanyika mjini Cape Town, Bw. Ramaphosa amesema, amani sio tu kutokuwepo vita, bali pia ni kutokuwepo hali isiyo na haki. Pia amehimiza kuunga mkono mageuzi mapya ya kutwaa ardhi bila fidia.
Bw. Ramaphosa amesema, ni lazima wajenge nchi ambayo fedha ziwe mali ya wananchi na ardhi idhibitiwe na wanaoitolea jasho, ili kutimiza amani endelevu nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |