• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala nchini Cameroon chatoa wito wa utulivu kabla ya matokeo rasmi ya kura ya urais kutangazwa

    (GMT+08:00) 2018-10-09 17:03:57

    Chama tawala nchini Cameroon (CPDM) kimetoa wito wa utulivu wakati nchi hiyo ikisubiri matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais uliofanyika jumapili iliyopita.

    Katibu mkuu wa chama hicho Jean Kuete amewataka wahusika wote kuendelea na majukumu yao na kuacha vitendo vyovyote vya uchochezi. Pia amemlaani mgombea urais kutoka upande wa upinzani Maurice Kamto kwa kujitangaza mshindi katika uchaguzi huo, na kueleza kushangazwa na hatua ya mgombea huyo.

    Kamati ya Kuhesabu Kura nchini Cameroon inatarajiwa kukusanya matokeo yote kwa ajili ya kuhesabu tena matokeo kwa mara ya mwisho.

    Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa kabla ya tarehe 22 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako