• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guinea yapenda kusukuma mbele uhusiano kati yake na China

    (GMT+08:00) 2018-10-09 17:15:29

    Rais Alpha Condé wa Guinea jana amesema, China ni mwenzi wake muhimu zaidi wa ushirikiano wa kimkakati, na Guinea inapenda kusukuma mbele uhusiano kati yake na China.

    Rais Condé amesema hayo wakati alipopokea hati za utambulisho za balozi mpya wa China nchini Guinea Bw. Huang Wei. Rais Condé amesema ushirikiano wenye ufanisi kati ya Guinea na China una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya jamii nchini Guinea. Pia ameeleza kuridhishwa na matokeo muhimu ya ushirikiano yaliyofikiwa na nchi hizo mbili kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako