• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe kufungua sekta ya madini ya Platinum kwa wawekezaji wote

    (GMT+08:00) 2018-10-09 19:10:05

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema serikali yake inakaribia kufungua sekta ya madini ya Platinum kwa wawekezaji wote wanaovutiwa nayo, na kwamba sera mpya ya kuongoza sekta ya almasi itatangazwa hivi karibuni.

    Rais Mnangagwa amesema, amenukuliwa na gazeti la The Herald la nchini humo akisema, kanuni ya umiliki wa asilimia 51-49 inayohusisha madini ya Platinum itafutwa hivi karibuni. Rais huyo amesema, awali nchi hiyo haikuwa na sera yoyote kuhusu almasi, lakini utafiti umefanyika na sera hiyo itatangazwa siku za karibuni.

    Zimbabwe ina hazina kubwa ya madini ya Platinum na hivyo kuifanya kuwa nchi ya pili duniani kwa madini hayo ikiifuata Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako