• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Hifadhi ya mafuta kujengwa kwa gharama ya dola milioni 51 Uganda

  (GMT+08:00) 2018-10-09 19:44:14

  Kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Uganda imepata kipande cha ardhi cha ekari 300 katika wilaya ya Wakiso ambapo itajenga hifadhi ya mafuta.

  Hifadhi hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 60 za bidhaa za petroli.

  Mkuu wa fedha kwenye kampuni hiyo Emmanuel Mugagga, amesema wanatafuta mshirika wa kujenga hifadhi hiyo inayotarajiwa kugharimu dola milioni 51.

  Hifadhi hiyo itatumika kama kituo cha kugawa bidhaa za petroli ambazo zitatokea kwenye kiwanda cha usafishaji wa bidhaa hiyo katika wilaya wa Hoima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako