• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wa Japan na Afrika wakubaliana kuchukua hatua za dharura za kisera

  (GMT+08:00) 2018-10-09 19:44:49

  Mawaziri wa Japan na wa Afrika wamekubaliana kuchukua hatua za dharura za kisera ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu barani humo.

  Wawakilishi kutoka nchi 52 za Afrika waliokutana mjini Tokyo Japan kwa mkutano wa mawaziri wa siku mbili walitambua changamoto zilizoko barani humo zikiwemo miundo mbinu, kutumia ipasavyo nguvu kazi, usalama na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Waziri wa mambo ya kigeni wa Japan Taro Kono amesema nchi za Afrika zinapiga hatua kwenye uwekezaji wa miundo mbinu lakini bado fedha zaidi zinahitajika ili kuunganisha nchi zaidi.

  Mkutano huo wa mawaziri wa Afrika nchini Japana unafanyika mbele ya mkutano wa 7 wa kimataifa kati ya pande hizo mbili TICAD utakaofanyika mjini Yokohama Agosti mwaka uajo.

  Mwaka 2016 Japan iliahidi kutoa msaada wa dola bilioni 30 kusaidia miradi ya serikali na sekta binafsi kwa kipindi cha miaka mitatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako