• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia: Ethiopia kutoa visa kwa waafrika wanapowasili

  (GMT+08:00) 2018-10-09 19:45:06

  Rais wa Ethiopia Mulatu Teshome ametangaza kuwa hivi karibuni serikali itaanzisha mpango wa kutoa visa kwa waru wote wa Afrika pindi tu wanapoingia nchini humo.

  Hiyo ina maana kuwa waafrika hawatahitaji kuomba visa kutoka balozi za Ethiopia zilizoko nchini kwao kabla ya kusafiri.

  Hatua hii inalenga kuongeza watalii na pia kuchochea ukuaji wa kiuchumi nchini humo.

  Rais Mulatu ameyasema hayo wakati wa kufunguliwa kwa kikao kipya cha bunge mjini Addis Ababa.

  Alisema kuwa na mpango kama huo kutasaidia Ethiopia kufungua zaidi fursa na kusaidia kamapuni kama vile shirika la ndege la Ethiopia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako