• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Angola wakubaliana kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo chanya kwa kasi

    (GMT+08:00) 2018-10-09 20:51:16
    Rais Xi Jinping wa China leo amefanya mazungumzo na rais João Manuel Gonçalves Lourenço wa Angola aliyeko ziarani hapa China.

    Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinatakiwa kuongeza kuaminiana kisiasa, kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu na ya kimkakati, kuelewana na kuungana mkono maslahi muhimu na masuala makubwa. Pia amesema kuwa inapaswa kutekeleza mafanikio yaliyopatikana katika mkutano wa viongozi wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, kuhimiza hatua zinazohusu "mipango kuhusu sekta nane muhimu", mchakato wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuimarisha uoanishaji wa mikakati ya maendeleo kati ya pande hizo mbili na ushirikiano katika maeneo ya jadi, huku zikihimiza ukuaji wa uchumi katika maeneo mapya, ili kuharakisha mchakato wa utandawazi wa viwanda na ukuaji wa uchumi wa Angola.

    Naye rais Lourenco ameeleza matumaini yake kwamba, ushirikiano kati ya Angola na China utakuwa mfano mzuri kwa ushirikiano kati ya Afrika na China, na Angola inazingatia umuhimu wa China katika mambo ya kimataifa, na kupenda kuimarisha ushirikiano kati yake na China katika mambo ya pande nyingi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako