• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yapiga marufuku maandamano ya kupinga kodi mpya

    (GMT+08:00) 2018-10-10 09:14:36

    Polisi wa Zimbabwe wamepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa kufanyika leo na shirikisho la wafanyakazi wa Zimbabwe ZTCU kupinga kodi ya asilimia mbili kwa miamala ya fedha ya kielektroniki iliyotangazwa hivi karibuni na serikali.

    Shirikisho hilo liliitisha maandamano hayo kupinga hatua hiyo, ambayo inalalamikiwa na wazimbabwe wengi, wanaoona kuwa tayari wanatozwa kodi kubwa.

    Sababu iliyotajwa na polisi kupiga marufuku hiyo, ni uamuzi wa kuzuia mikusanyiko yote ya umma kutokana na tahadhari iliyotolewa dhidi ya hatari ya ugonjwa wa kipindupindu, ambacho mpaka sasa kimesababisha vifo vya watu 49.

    Polisi wameonya kuwa kama vurugu zitatokea kutokana na kuzuia maandamano hayo, shirikisho la wafanyakazi ndio litawajibika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako