• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema imeanza kujenga miundo mbinu ya magari ya umeme

    (GMT+08:00) 2018-10-10 09:14:54

    Serikali ya Kenya imesema imeanza kujenga miundo mbinu ya magari ya umeme, ili kusaidia kupunguza mzigo wa magari yanayotumia mafuta.

    Meneja msaidizi wa mamlaka ya ukaguzi na usalama wa magari ya Kenya (NTSA) Bw. Opere Nyarora amesema serikali inaandaa vigezo ili kujiweka tayari kwa ajili ya uzinduzi.

    Amesema kwa sasa serikali iko kwenye mchakato wa kutoa mafunzo kwa wakaguzi wa magari, na vituo viwili kwa ajili ya magari hayo vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni mjini Nairobi na Mombasa.

    Bw. Nyarora amesema serikali ya Kenya imefikia hatua hiyo kutokana na ushauri iliopata kutoka kwa shirika la mazingira la umoja wa mataifa, ili kupunguza uchafuzi wa hewa unaowaathiri watu wasiojua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako