• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa IMF asisitiza kuangalia ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mtizamo mpana zaidi

    (GMT+08:00) 2018-10-10 10:27:14

    Mkurugenzi wa idara ya Afrika ya Shirika la fedha la kimataifa IMF Bw. Abebe Aemro Selassie, amesisitiza umuhimu wa kuuangalia ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mtizamo mpana na wa maendeleo.

    Akizungumzia shutuma zilizotolewa hivi karibuni na nchi za magharibi dhidi ya China, kuwa misaada ya China kwa Afrika imezisababishia nchi za Afrika kuwa na msukosuko wa madeni, Bw. Selassie amesema hivi sasa nchi sita au saba za Afrika zinakabiliwa na hatari ya kuingia kwenye msukosuko wa madeni, na mikopo ya nchi hizo imetolewa na mashirika na nchi mbalimbali, sio China peke yake. Amesema mikopo yote iliyotolewa na China imesaidia kukidhi mahitaji makubwa ya nchi zinazoipokea mikopo hiyo.

    "mikopo iliyotolewa na China kwa ajili ya miradi mikubwa ya miundombinu barani Afrika, ikiwemo bandari, barabara na reli, mingi ni mikopo ya muda usiozidi mwaka mmoja, ni muhimu kwa nchi za Afrika kutafuta njia yenye uwiano. Ni wazi kwamba miradi mingi ya miundombinu iliyojengwa kwa ufadhili wa China, imekidhi mahitaji ya dharura. Muhimu zaidi ni kwamba, miradi hiyo yote inaleta faida kubwa ya kutosha, ili nchi zilizopokea mikopo ziweze kulipa madeni yao. Kama mikopo hiyo imetumiwa kufadhili miradi yenye faida kubwa, basi mikopo hiyo ina manufaa makubwa kwa nchi zinazopokea, tunatakiwa kuuangalia ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mtizamo mpana zaidi."

    Bw. Abebe amesema anaamini kuwa nchi za Afrika zinaweza kupata uwiano kati ya kutimiza maendeleo endelevu, na kupunguza hatari ya madeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako