• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbwana Samatta: Tetesi zasema atatua Uingereza mwezi Januari

  (GMT+08:00) 2018-10-10 10:43:56

  Habari kubwa kutoka nchini Ubeligiji ni kwamba Huenda msimu ujao mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya Genk akahamia ligi kuu ya Uingereza katika dirisha la usajili la mwezi Januari

  Hii inatokana na ripoti ya mtandao wa HITC ambao umeandika kuwa saini ya Samatta mchezaji inawindwa na klabu Zaidi ya tano za Uingereza zikiwemo West Ham United, Everton na Burnley.

  Klabu zote hizo zimevutiwa na ubora wa kiwango kilichoonyeshwa na Samatta tangu ajiunge na Genk na Zaidi katika msimu huu wa ligi kuu ya Ubelgiji, lakini pia michuano ya Yuropa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako