• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yalaumu upungufu wa fedha kwa ajili ya wakimbizi wa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-10-10 16:44:24

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limelaumu upungufu wa fedha za kuwahudumia wakimbizi wa Somalia na watu wengine waliokimbia makazo yao nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa jana na Shirika hilo imesema, dola milioni 522 za kimarekani zilizohitajika kusaidia hali nchini Somalia, ni asilimia 37 tu ya fedha hizo ndio imepatikana. Taarifa hiyo pia imesema, baada ya miongo kadhaa ya mapigano, Somalia imepata maendeleo, lakini hali bado ni tete na inahitaji msaada zaidi.

    Shirika hilo limesema, zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Somalia wamepewa hifadhi katika nchi sita na wengine milioni 2 wamepewa hifadhi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako