• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 50 wafariki katika ajali ya barabarani kaskazini magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-10-10 16:45:08

    Watu 50 wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani inayohusisha basi la abiria iliyotokea mapema leo kwenye barabara kuu ya Kisumu-Muhoroni, eneo la Fort Tenan lililoko kaunti ya Kericho, kaskazini magharibi mwa Kenya.

    Kamanda wa polisi wa kanda ya Bonde la Ufa Francis Munyambu amesema, watu 42 walifariki papo hapo huku wengine wanane wamefariki katika hospitali walipokuwa wakipata matibabu, na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

    Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kericho James Mugera amesema, kazi ya uokoaji bado inaendelea, na kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka kwa kuwa bado kuna watu wamekwama kwenye mabaki ya basi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako