• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya Bw. Mike Pence yawachekesha watumiaji wa mtandao wa Internet nchini China

    (GMT+08:00) 2018-10-10 16:56:05

    Katika siku saba zilizopita za mapumziko wakati wa Siku ya taifa la China, makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence alitoa hotuba inayosifu uwezo mkubwa wa Marekani huku "ikichochea tamaa ya makuu ya China". Hotuba hiyo si kama tu imekosolewa na watumiaji wa mtandao wa Internet nchini Marekani, bali pia imekosolewa nchini China baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kichina na kutangazwa kupitia tovuti ya Wechat ya Ubalozi wa Marekani nchini China.

    Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa China wamesema, "Kitendo cha Bw. Pence kisicholingana na hali ya kawaida kabla ya uchaguzi wa kipindi cha kati kinaonesha wasiwasi wa serikali ya Marekani". Mbali na hayo, aliyosema Bw. Pence hayalingani na ukweli wa mambo, na yamewachekesha wachina.

    Kwa mfano kama Bw. Pence alivyotaja na kuwastaajabisha watu ni aliposema, "katika miaka mitano baada ya nchi zetu mbili kukabiliana na maadui bega kwa bega, tulipambana katika Peninsula ya Korea. Baba yangu alikuwa mstari wa mbele kwenye vita hiyo inayolenga kulinda uhuru". Lakini jambo linalotia shaka kwa wachina ni kwamba, baba wa Bw. Pence hakumwambia kuwa ni baada ya jeshi la Marekani kuzusha vita kwenye sehemu ya Kaskazini Mashariki mwa China, ndipo jeshi la ukombozi wa watu wa China lilianzisha mapambano ya kujilinda. Wachina wamepinga kithabiti hadithi hiyo ya kupotosha ukweli wa mambo, iliyotungwa na Bw. Pence.

    Mbali na hayo, Bw. Pence alisema "Katika miaka 25 iliyopita Marekani iliijenga upya China". Lakini katika miaka 25 iliyopita, China ilijipatia njia ya kufanya mageuzi na ufunguaji mlango, wakati Marekani na baadhi ya nchi za magharibi zilikuwa zikisherehekea kusambaratika kwa Urusi, kutoa kauli ya "Tishio la China", na kujaribu kuivuruga China. Pato la taifa la China lililoongezeka kutoka dola bilioni 57 za kimarekani la mwaka 1992 hadi dola trilioni 11.99 za kimarekani la mwaka 2017, lilipatikana kwa juhudi za wachina kutokana, na kuwa China ilijifufua mara nyingi katika historia ya maelfu kadhaa iliyopita bila kuingiliwa, na hata hakuna nguvu ya nje iliyokuwa na uwezo wa kujenga upya nchi hii yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Kama Marekani iliweza kuijenga upya China kwa urahisi, basi isingekuwa vigumu kwake kuzijenga upya Iraq, Afghanistan na Syria, si ndiyo? Ndiyo maana wachina hawatakubali Marekani kujirembusha kwa kupora juhudi kubwa zilizofanywa na wachina.

    Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wa China wameeleza kuwa, China inajihusisha na mambo mengi yanayotokea katika mchakato wake wa kujiendeleza na haina muda wa kutosha, pia wameishauri serikali ya China ishirikiane na wale walio na nia ya dhati ya ushirikiano. Endapo kuna watu wanaotaka kuzusha migogoro, wachina hakika watajilinda na kujibu bila kusita, kwani hakuna vitu vinavyoweza kuzuia hatua ya watu bilioni 1.4 katika kujitafutia maisha mazuri!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako