• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza kulinda kithabiti mfumo wa pande nyingi ili kuboresha mazingira ya maendeleo ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-10-10 18:28:46

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amezihimiza nchi mbalimbali kulinda kithabiti mfumo wa pande nyingi, ili kuboresha mazingira ya maendeleo ya kimataifa.

    Bw. Ma amesema hayo katika mjadala wa kawaida wa kamati ya pili ya Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa. Amesema, hivi sasa kanuni za biashara za kimataifa zinaathiriwa vibaya, na mfumo wa pande nyingi ambao ni msingi wa maendeleo endelevu unakabiliwa na changamoto. Kulinda kithabiti mfumo huo na kupinga hatua ya upande mmoja kunahusiana na maendeleo ya nchi mbalimbali hasa maendeleo endelevu ya nchi zinazoendelea.

    Bw. Ma amezitaka pande mbalimbali kuchukua hatua halisi kulinda mfumo wa kimataifa unaofuata kanuni za Umoja wa Mataifa, na kulinda mfumo wa biashara za pande nyingi kuendana na Shirika la Bishara la Kimataifa WTO, ili kuimarisha usimamizi wa uchumi wa dunia nzima na kujenga mazingira mazuri ya maendeleo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako