• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Uganda,Yoweri Museveni awahimiza waganda kufanya kilimo cha umwagiliaji

  (GMT+08:00) 2018-10-10 20:01:06

  Rais wa Uganda ,Yoweri Museveni,jana aliwahakikishia waganda kwamba serikali yake imejitolea kukuza umwagiliaji na kuhakikisha utoshelevu wa chakula nchini humo.

  Akizungumza kwenye maadhimisho ya 56 ya Sherehe za Uhuru katika kiwanja cha Kasasa katika wilaya ya Kyotera jana,alisema mwkaa huu wa fedha,serikali yake itazindua miradi ya umwagiliaji katika wilaya 14.

  Museveni alisema wakulima watakapokumbatia kilimo cha umwagiliaji,watapiga jeki uzalishaji wa chakula na kupunguza changamoto za mabadiliko ya tabianchi zinazoonekana wakati wa kiangazi.

  Aidha litoa wito kwa wakulima kuachana na kilimo cha ustawi na kuanza kilimo biashara.

  Alisema kuwa anasikitishwa kuona kwamba sekta ya kilimo inakua kwa kiwango kidogo cha asilimia 3.2 kwa mwaka ikilinganishwa na teknolojia ya habari na mawasiliano asilimia 7.9 ,huduma 7.3% na viwanda 6.2%.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako