• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Angola zakubaliana kuimarisha ushirikiano

  (GMT+08:00) 2018-10-10 20:01:30

  Rais wa China Xi Jinping jana alifanya mazungumzo na Rais wa Angola Joao Lourenco ambaye yuko ziarani Beijing ,ambapo walikubaliana kuendeleza mahusiano ya nchi hizo mbili.

  Xi alisema ana furaha kwa ujio wa mara ya pili wa Rais Lourenco nchini China katika kipindi cha mwezi mmoja ,ambaye alihudhuria Mkutano wa Kilele wa ushirikiano wa China na Africa,FOCAC,mapema mwezi Septemba.

  Xi alisema mafanikio ya mkutano huo yameleta ari na fursa katika maendeleo ya ushirikiano wa China na Afrika nan a China na Angola,akitoa wito kwa pande hizo mbili kukuza maendeleo ya ushirikiano huo.

  Rais wa Angola Joao Lourenco alisema kuwa China na Angola zimeendeleza mabadilishano ya ngazi za juu,ishara kuwa pande hizo mbili zinazingatia mno mahusiano hayo.

  Marais hao wawili pia walishuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako