• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viwanda vya kuchakata mbaazi na choroko kujengwa Arusha na Dar es Salaam

  (GMT+08:00) 2018-10-10 20:01:46

  Wawekezaji wamejitokeza kuwekeza katika viwanda vya kuchakata mazao ya mbaazi na choroko nchini Tanzania.

  Viwanda hivyo vinatarajiwa kujengwa katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro,na vitatumia mbaazi na choroko kutoka kwa wakulima kwa ajili ya kutengeneza bidha mbalimbali zitakazouzwa ndani na nje ya nchi.

  Matumaini hayo kwa wakulima yalitolewa jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo,Omari Mgumba, ambapo amesema kilimo kinategemewa na watanzania wengi na juhudi za kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao la mbaazi ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda.

  Alisema serikali imeamua kuchukua hatua kwa kuwahamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika mazao nchini Tanzania, jambo ambalo limeanza kutekelezwa.

  Amebainisha kuwa hatua hiyo ni kujibu kero ya muda mrefu ya wakulima wa mazao hayo katika mikoa ya Manyara, Arusha, Dodoma na maeneo mengine kukosa soko la uhakika kwa kuongeza thamani ya mazao hayo nchini humo.

  Aidha Mgumba alisema kwa kuongeza thamani ya mbaazi kunapanua soko soko katika dunia badala ya kutegemea soko moja tu la nchini India, ambapo sasa mbaazi zitauzwa nchi mbalimbali zikiwemo nchi za Kiarabu, Ulaya na Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako