• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IMF yasema uchumi wa Dunia umeshuka

  (GMT+08:00) 2018-10-10 20:02:08

  Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema vita vya kibiashara kati ya Marekani na China pamoja na madeni makubwa vimeshusha uchumi wa dunia.

  Utafiti kuhusu hali ya uchumi Duniani uliotangazwa na IMF jana,ulionyesha kuwa ukuaji wa uchumi duniani mwaka huu utasalia katika kiwango cha asilimia 3.7 na kuzidi kusalia katika kiwango hicho mwakani.

  Utafiti huo unaonyesha kuwa kiwango hicho ni cha chini ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3.9 uliotangazwa Aprili.

  Akizungumza wakati wa kutangazwa kwa Ripoti hiyo,Mchumi Mkuu wa IMF Mary Obstfeld alisema uchumi unaonekana kuporomoka na kuwa katika kiwango cha asilimia 3.7.

  Aidha IMF pia inasema kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mataifa ya China na Marekani yaliyo na uchumi mkubwa duniani nacho pia kimeshuka.

  Mkutano wa Kilele wa IMF utafanyika Bali,Indonesia kuanzia tarehe 12 hadi 14 Oktoba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako