• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Sudan aahidi kutatua msukosuko wa upatikanaji wa fedha

    (GMT+08:00) 2018-10-11 08:42:28

    Waziri mkuu wa Sudan Bw. Mutaz Mussa ametangaza kuwa msukosuko wa upatikanaji wa fedha nchini Sudan utatatuliwa, na mashine za kutolea fedha ATM zitawekwa pesa kabla ya Jumamosi.

    Bw. Mussa ambaye pia ni waziri wa fedha wa Sudan, amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa amepata uhakikisho kutoka kwa gavana wa Benki kuu ya Sudan kwamba mashine zote za ATM zitawekwa pesa kabla ya Jumamosi ijayo.

    Tangu mwezi Februari, Sudan imekuwa inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa fedha taslim, kufuatia kushuka thamani kwa paundi ya Sudan dhidi ya dola ya kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako