• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaanza kutoa hati za kusafiria zinazosomwa kwa mashine

    (GMT+08:00) 2018-10-11 08:42:48

    Serikali ya Rwanda imeanza kutoa hati za kusafiria zinazosomwa kwa mashine kwa wakimbizi nchini humo, ambazo zitawawezesha kusafiri kwa uhuru.

    Akizungumza kwenye hafla ya kuzindua hati hiyo mpya ya kusafiria iliyofanyika jana mjini Kigali, waziri wa wakimbizi wa Rwanda Bibi De Bonheur Jeanne D'Arc amesema kutolewa kwa hati hizo za kusafiria, zitatoa athari chanya kwa maisha ya wakimbizi na kuhalalisha safari zao za kuvuka mipaka.

    Utoaji wa hati hizo utatekelezwa na wizara ya usimamizi wa majanga na wakimbizi ya Rwanda, Kurugenzi kuu ya uhamiaji ya Rwanda na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

    Kwa mujibu wa wizara ya wakimbizi ya Rwanda, hivi sasa nchi hiyo imepokea wakimbizi laki 1.53, wengi wao wakiwa wanatoka Burundi na DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako