• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Erdogan ataka nchi za Afrika kutumia sarafu zao katika biashara na Uturuki

    (GMT+08:00) 2018-10-11 08:45:57

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametoa wito kwa nchi za Afrika kutumia sarafu zao katika kufanya biashara na Uturuki, akisema hii ni kwa ajili ya kupunguza hatari zinazotokana na sarafu za kigeni.

    Akiongea katika kongamano la uchumi na biashara kati ya Uturuki na Afrika mjini Istanbul, rais Erdogan amesema Uturuki hivi karibuni inakabiliwa na shambulizi la kuilenga, aliloliita "shambulizi la kiuchumi" kutoka nchi za nje, ambalo limesababisha kuzorota kwa thamani ya sarafu ya Uturuki Lira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako